• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • NFF yashtushwa na hatua ya FIFA kumfungia maisha kocha Siasia

  (GMT+08:00) 2019-08-21 08:14:13
  Shirikisho la soka nchini Nigeria (NFF), limeshtushwa na hatua ya Shirikisho la soka duniani (FIFA) kumfungia maisha kocha wa zamani Samson Siasia, kutojihusisha na masuala ya soka.

  FIFA ilitangaza kuchukua hatua hiyo, baada ya kumshutumu kocha Siasia kwa kujihusisha na rushwa katika nyakati tofauti, madai ambayo ameyakanusha.

  Uongozi wa NFF umeeleza kuwa, utahakikisha kumsaidia kocha huyo aliyeiongoza nchi hiyo katika michezo ya Olimpiki mwaka 2016 kusafisha jina lake baada ya adhabu hiyo ya FIFA.

  FIFA imesema, Siasia mwenye umri wa miaka 52, alishirikiana kwa karibu na Wilson Raja Perumal raia wa Singapore, anayehusishwa na upangaji wa matokeo ya mechi kadhaa za Kimataifa, kinyume na kanuni za FIFA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako