• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shanghai yavumbua njia ya kuvutia watu wenye uwezo ili kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu

    (GMT+08:00) 2019-08-21 16:51:16

    Mji wa Shanghai ni mtangulizi wa utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango na maendeleo yenye sifa ya juu. Wakati mji huo unahimiza maendeleo yenye sifa ya juu, pia unafanya majaribio na uvumbuzi katika nyanja mbalimbali, haswa namna ya kuvutia watu wenye uwezo.

    Tarehe 18 Aprili mwaka 1990, serikali ya China ilianzisha mkakati wa kuendeleza eneo la Pudong mjini Shanghai, na kulifanya liwe dirisha la mageuzi na kufungua mlango. Bw. Zhao Qizheng aliyekuwa naibu meya wa Shanghai na mkurugenzi wa kwanza wa mamlaka ya uendeshaji ya eneo hilo anasema,

    "Kwa nini tuliamua kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango mjini Shanghai? Kwa sababu marekebisho ya mambo ya mji huo hayakuweza kucheleweshwa tena. Sekta za uchumi zilitakiwa kurekebishwa, huku wakazi wa Shanghai wakihitaji kuhamasishwa. Hivyo sera yetu ya kuendeleza eneo la Pudong ilipongezwa na watu."

    Katika miaka 29 iliyopita, thamani ya uzalishaji mali wa eneo la Pudong imeongezeka na kufikia dola za kimarekani bilioni 142 hivi sasa kutoka dola milioni 852 ya mwaka 1990. Mkakati wa kuendeleza Pudong umetia uhai mpya maendeleo ya Shanghai, na kuuhimiza mji huo kuwa kitovu cha kimataifa cha fedha, biashara na uchumi.

    "Kuhimiza uendelezaji wa kiwango cha juu zaidi kupitia watu wenye uwezo wa kiwango cha juu zaidi", ni wazo la siku zote la serikali ya Shanghai katika kuendeleza eneo la Pudong. Hivi sasa wageni wakitaka kufanya kazi mjini Shanghai, wanatakiwa kutoa ombi mara moja tu, ambalo litapitishwa ndani ya siku tano za kazi. Naibu meya wa Shanghai Bw. Chen Yin anasema,

    "Ili kuanzisha mazingira mazuri zaidi ya kuvutia watu wenye uwezo kutoka sehemu nyingine za China na hata nchi za nje, tulitoa sera 12 mpya, na pia tumeanzisha mfuko wa fedha wenye zaidi ya dola za kimarekani bilioni 14 unaoshughulikia watu wenye uwezo wa hali ya juu na ujenzi wa miundombinu."

    Bw. Ni Wenjie ni mfanyakazi wa Kampuni ya Yaoming Kangde ya Shanghai, na anashughulikia kuandikisha wafanyakazi wapya. Amesema sera mpya ya Shanghai imeongeza ufanisi wa kuwaajiri wafanyakazi kutoka sehemu nyingine, akisema,

    "Kutokana na sera mpya, watu wengi wanaotaka kufanya kazi mjini Shanghai wamepunguza wasiwasi wao. Hivyo sasa ni rahisi zaidi kwetu kuwaajiri wafanyakazi wapya kuliko zamani."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako