• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapendekeza mwaka kesho kuwa mwaka wa ushirikiano wa uvumbuzi kati ya China, Japan na Korea Kusini

    (GMT+08:00) 2019-08-21 19:07:07

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi leo ameendesha mkutano wa 9 wa mawaziri wa mambo ya nje wa China, Japan na Korea Kusini uliofanyika hapa Beijing.

    Bw. Wang amesema, mkutano huo umepata mafanikio makubwa. Pande hizo tatu zimekubali pendekezo la China kuchukua mwaka kesho kuwa mwaka wa ushirikiano wa uvumbuzi kati yao. Ikiwa ni nchi mwenyekiti, China inapenda kudumisha mawasiliano na Korea Kusini na Japan na kushirikiana kwa pamoja kufanya maandalizi ya mkutano wa mwaka huu wa viongozi wa nchi hizo tatu.

    Bw. Wang pia amesema, ushirikiano kati ya nchi hizo tatu unapaswa kuwa msingi wa ustawi na utulivu wa kaskazini mashariki mwa Asia. Zinapaswa kushirikiana kulinda mfumo wa biashara huru, kujenga uchumi unaofungua mlango wa dunia na kutoa nguvu mpya kwa ongezeko la uchumi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako