• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • KUOGELEA: Mashindano ya dunia Hungary- Mtanzania ang'ara

  (GMT+08:00) 2019-08-22 07:49:27

  Nahodha wa timu ya taifa ya vijana ya kuogelea ya Tanzania Dennis Mhini ameng'ara katika mashindano ya dunia ya kuogelea mjini Budapest Hungary baada ya kuongoza katika kundi la kwanza.

  Dennis ambaye ni mwanafunzi wa shule ya St. Felix ya Uingereza, alifanya vyema kwenye mashindano ya mita 100 katika mtindo wa backstroke kwa kutumia muda wa 1.04.27 na kuwashinda wenzake toka Pakistan, Madagascar na Sudan.

  Mara baada ya shindano hilo Dennis amesema, amefurahi kushinda na kuwakilisha vyema Tanzania kwenye mashindano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako