• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Russia yachukua hatua kukabiliana na mvutano kutoka upande wa magharibi

  (GMT+08:00) 2019-08-22 14:29:31

  Waziri wa Ulinzi wa Russia Bw. Sergey Shoigu amesema nchi hiyo itachukua hatua kukabiliana na mvutano unaoletwa na nchi za magharibi, ikiwemo NATO kuongeza nguvu ya kijeshi Ulaya Mashariki, Marekani kuweka mifumo ya ulinzi dhidi ya makombora nchini Poland na Romania, na NATO kuongeza ushirikiano wa kijeshi kati yake na Finland na Sweden.

  Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi ya Russia imesema, kabla ya mwisho wa mwaka huu, eneo la kijeshi la magharibi mwa nchi hiyo litapokea zana mpya za kijeshi zaidi ya 1,300 na kuendelea kuongeza idadi ya wanajeshi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako