• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China

    (GMT+08:00) 2019-08-22 17:02:23

    Serikali ya China imetoa waraka wa kuunga mkono kuujenga mji wa Shenzhen kuwa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China, na kuutaka mji huo kuhimiza ujenzi wa eneo kubwa la ghuba ya Guangdong, Hong Kong na Macao.

    Eneo kubwa la ghuba ya Guangdong, Hong Kong na Macao linaundwa na Hongkong, Macao, na miji tisa ya mkoa wa Guangdong ikiwemo Guangzhou, Shenzhen na Zhuhai. China inapanga kulijenga eneo hilo liwe kundi la majiji ya kimataifa, kitovu cha kimataifa cha uvumbuzi wa sayansi na teknolojia, uungaji mkono wa ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kielelezo cha ushirikiano kati ya China bara na Hong Kong pamoja na Macao. Waraka uliotolewa na serikali kuu ya China umesema, ujenzi wa eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China mjini Shenzhen utasaidia kutekeleza mkakati wa eneo kubwa la ghuba ya Guangdong, Hong Kong na Macao, na kuendeleza sera ya "nchi moja, mifumo miwili". Naibu mkuu wa taasisi ya utafiti wa maendeleo ya China Bw. Wu Jian amesema, kutolewa kwa waraka huo kunamaanisha kuwa mji wa Shenzhen umekuwa injini kuu ya maendeleo ya eneo kubwa la ghuba ya Guangdong, Hong Kong na Macao, akisema,

    "Kufuatia waraka huo, mji wa Shenzhen unaongoza miji 11 ya eneo hilo. Utaongoza maendeleo ya miji hiyo na kuhimiza ushirikiano kati ya miji ya Guangdong na Hong Kong pamoja na Macao, na kutoa mchango mkubwa kwa maendeleo ya sehemu hiyo."

    Mkurugenzi wa kituo cha utafiti wa utalii na nyumba cha taasisi ya utafiti wa maendeleo ya China Bw. Song Ding anaona kuwa, ukiwa mtangulizi wa utekelezaji wa sera ya mageuzi na kufungua mlango, mji wa Shenzhen una uwezo wa kutosha, akisema,

    "Katika miaka 40 iliyopita tangu China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na kufungua mlango, mji wa Shenzhen umepata mafanikio makubwa zaidi ukilinganishwa na miji mingine ya China. Hivyo serikali kuu ya China imeamua kuufanya uwe mtangulizi tena katika duru mpya ya mageuzi."

    Waraka huo pia umeutaka mji wa Shenzhen uongeze mawasiliano na ushirikiano na Hong Kongo na Macao, na kuwapa watu wa Hong Kong na Macao haki sawa na wakazi wa Shenzhen.

    Bw. Huang kutoka Hong Kong ni mjasiriamali kutoka mkoa wa Shenzhen, anasema,

    "Mji wa Shenzhen una fursa nyingi, rasilimali kubwa na majukwaa mazuri. Naona unawavutia sana watu kutoka sehemu nyingine."

    Mkuu wa Chuo Kikuu cha Gongkai cha Hongkong Bw. Huang Yushan anaona watu wa Hong Kong watanufaika na eneo la kielelezo cha ujamaa wenye umaalum wa China, na Hong Kong inapaswa kuchukua fursa hii kuongeza ushirikiano na Shenzhen.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako