• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matakwa makubwa zaidi ya watu wa China kwa hali ya Hong Kong ni kuzuia vurugu na mabavu na kurejesha utaratibu

    (GMT+08:00) 2019-08-22 18:15:19

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang amesema, matakwa makubwa zaidi ya watu bilioni 1.4 wa China wakiwemo ndugu wa Hong Kong ni kuzuia vurugu na mabavu na kurejesha utaratibu, huku matarajio yao makubwa zaidi ni kulinda ustawi na utulivu wa Hong Kong.

    Habari zinasema, baadhi ya wachina wanaoishi na kusoma katika nchi za nje zikiwemo Uingereza na Australia wameshiriki kwenye maandamano ya kuunga mkono msimamo wa serikali ya China kuhusu Hong Kong. Hata hivyo baadhi ya serikali za nchi za nje zina wasiwasi kwamba shughuli hizo zinaandaliwa na ofisi za China katika nchi za nje. Akifafanunua kuhusu hilo Bw. Geng anasema,

    "katika baadhi ya miji ya nchi za nje, wachina wanaoishi na kusoma ng'ambo wameandamana barabarani, kueleza matarajio na matakwa ya kuunga mkono umoja wa kitaifa na kulinda ustawi na utulivu wa Hong Kong. Wachina hao kuonesha hasira na upinzani kwa vitendo vya kujaribu kufarakanisha taifa na kupaka matope taswira ya China ni jambo linaloeleweka. Tunawataka wachina wanaoishi katika nchi za nje kuonesha uzalendo wao kwa njia inayofaa na kuzingatia kulinda usalama wao wenyewe. "

    Bw. Geng pia amesema, serikali ya China siku zote inawataka raia wake wanaoishi katika nchi za nje kufuata sheria za huko, na kuzisihi nchi husika kuheshimu na kuelewa shughuli halali za raia hao na kuhakikisha na kulinda maslahi yao halali. Anasema,

    "Unauliza kama shughuli hizo zinaandaliwa na ofisi za China katika nchi za nje au la, naweza kukujibu kwa uwazi kuwa, hivi sasa matakwa makubwa zaidi ya watu bilioni 1.4 wa China wakiwemo ndugu wa Hong Kong ni kuzuia vurugu na mabavu na kurejesha utaratibu, huku matarajio yao makubwa zaidi ni kulinda ustawi na utulivu wa Hong Kong. Hii ni nia ya pamoja ya watu wote wa China, unadhani nia ya watu bilioni 1.4 inaweza kushirikishwa na kudhibitiwa?"

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako