• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Safari ya kwanza ya shirika la ndege la Uganda kugharimu $45 kwenda Nairobi

  (GMT+08:00) 2019-08-22 19:17:24

  Shirika la ndege la Uganda limepunguza nauli ya safari yake ya kwanza itakayokuwa tarehe 28 Agosti,huku nauli ya tiketi ya njia moja ikigharimu Shs166,000 (sawa na usd 45) kutoka Entebbe hadi uwanja wa JKIA jijini Nairobi.

  Hii inamaanisha kuwa tiketi ya kwenda na kurudi itauzwa kwa Shs330,000 (USD90),kutoka bei ya kawaida ya wsatani wa $300 (UgShs1.1 million) ambayo mashirika mengine ya ndege yanalipisha.

  Tovuti ya shirika hilo la ndege hivi sasa inaonyesha kuwa hakuna ushuru wowote uliowekwa katika nauli hiyo.Ushuru ukijumuishwa nauli hiyo huenda ikaongezeka kwa $147 (Shs542,000) na kufanya gharama zote za nauli kufika $192 (Shs709,000) kwa safari ya njia moja.

  Aidha tovuti hiyo inaonyesha kuwa safari ya kwenda na kurudi itagharimu $277 (Shs102,000) ikiwa pamoja na ushuru.

  Haijabainika ushuru utaanza kutozwa lini.Ukataji tiketi kwa njia ya kielektroniki ulianza jana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako