• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yazindua mfumo wa ndani wa ulinzi

    (GMT+08:00) 2019-08-23 08:27:59

    Rais Hassan Rouhani wa Iran amepongeza kuongezeka kwa nguvu ya nchi hiyo dhidi ya shinikizo linaloongezeka la Marekani, na kusema nchi yake haijawahi kusikitishwa kutokana na njama za adui, bali imesimama dhidi yao kwa nguvu zaidi.

    Rais Rouhani amesema hayo katika hafla ya kuzindua mfumo wa makombora ya ulinzi wa anga aina ya Bavar-373 iliyofanyika jana. Amesema shinikizo la Marekani dhihi ya Iran limeshindwa, na kuwapongeza wataalam wa Iran kwa kusanifu na kujenga mfumo huo.

    Waziri wa ulinzi wa Iran ambaye pia alihudhuria hafla hiyo Bw. Amir Hatami amesema Iran imefanikiwa kutengeneza mfumo makini ambao sio tu unakabiliana na matishio ya anga, bali pia unatambua, kufuatilia, na kuharibu ndege na makombora yanayoweza kukwepa rada.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako