• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kitendo cha Marekani kuitumia China kama sababu ya kujitoa INF hakikubaliki

    (GMT+08:00) 2019-08-23 08:28:21

    Balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Zhang Jun, amesema kuitumia China kama sababu ya Marekani kujitoa kwenye Mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati (INF) ni kitendo ambacho hakikubaliki.

    Akizungumza katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana, Balozi Zhang amesema China inapinga tuhuma zisizo na msingi zinazotolewa na Marekani, na kuongeza kuwa China inafuatilia sera ya ulinzi wa taifa ambayo asili yake ni kujilinda.

    Aidha, amesema mkakati wa nyuklia wa China kwa ajili ya kujilinda ni wa wazi na inawajibika juu ya sera yake ya nyuklia. Kwa miongo kadhaa, China imeshiriki katika mazungumzo na majadiliano ya kudhibiti silaha chini ya mfumo wa pande nyingi, na inapinga kithabiti mashindano ya kisilaha na kufanya juhudi kulinda utulivu na usawa wa kimkakati duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako