• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi wa Kenya nchini China atarajia injini mpya ya ushirikiano kati ya nchi hizo

  (GMT+08:00) 2019-08-23 18:21:33

  Balozi wa Kenya nchini China Sarah Serem amesema, Kenya inatumai kujifunza na kuiga kwa makini uzoefu wa maendeleo ya China, na kuleta injini mpya kwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

  Tangu China na Kenya zianzishe uhusiano wa kibalozi miaka 56 iliyopita, ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika nyanja za siasa, uchumi na jamii umefikia mafanikio makubwa. Balozi Serem amesema Kenya inastahili kujifunza uzoefu wa maendeleo wa China. Anasema,

  "Tunastahili kujifunza uzoefu wa maendeleo ya China katika miaka 70 iliyopita tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China. China imeboresha miundombinu, kuinua kiwango cha maisha ya watu, na kuendeleza sekta ya viwanda kwa kasi. Hayo yote ni mafanikio tunayoweza kuiga."Hivi sasa nchi za Afrika zinasukuma mbele mafungamano ya uchumi barani Afrika, huku pendekezo la China la "Ukanda Mmoja, Njia moja" likihamasisha maingiliano ya kikanda ya uchumi na biashara. Reli ya SGR inayounganisha Mombasa na Nairobi nchini Kenya ni mradi uliotekelezwa na kampuni ya China kufuatia pendekezo hilo, na inatarajiwa kuunganisha nchi sita za Afrika Mashariki katika siku zijazo. Balaozi Serem amesema hivi sasa reli hiyo inachangia sana uchumi wa Kenya. Anasema,

  "Reli ya SGR ni mafanikio makubwa zaidi tuliyopata ndani ya muda mfupi. Si kama tu imetia nuru kwa nchi yetu, bali pia imehimiza uchumi wetu."

  Hivi sasa kutokana na ongezeko la vitendo vya upande mmoja, kujilinda kibiashara na umwamba, mfumo wa pande nyingi unakabiliwa na changamoto kubwa. Balozi Serem amesema rais Xi Jinping wa China ametetea mara nyingi wazo la jumuiya yenye hatma ya pamoja. Kenya inapenda kuwa pamoja na China kulinda mfumo wa pande nyingi, na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya China na Afrika. Anasema,

  "Naona dunia nzima ni familia moja, na ni jumuiya yenye hatma ya pamoja. Endapo tu nchi zote duniani zitapata maendeleo, ndipo dunia itapata maendeleo ya kweli. China inatakiwa kushikamana na dunia yote ili kuhimiza usawa wa binadamu. Pia naipongeza China kwa kupenda kutafuta maendeleo ya pamoja na nchi za Afrika, na huu ni ushirikiano wa kunufaishana."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako