• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yatarajia kuiuzia China maparachichi mabichi

    (GMT+08:00) 2019-08-23 18:22:54

    Balozi wa Kenya nchini China Bi. Sarah Serem amesema, Kenya inafanya mazungumzo na China kuhusu kuiuzia maparachichi mabichi, baada ya kutambua makubaliano ya zamani hayawezi kuwanufaisha wakulima wadogo wa Kenya.

    Akizungumza na waandishi wa habari jijini Beijing, China, Bi. Serem amesema nchi hizo mbili zinafanya kazi kwa pamoja ili kuhimiza biashara ya kunufaishana kati yao.

    Kenya ni nchi ya pili barani Afrika baada ya Afrika Kusini kwa kilimo cha maparachichi. Maelfu ya wakulima waliopanda kahawa sasa wamegeukia kupanda miti ya maparachichi, inayojulikana kama "dhahabu ya kijani".

    Kwenye mkutano wa pili wa kilele wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" uliofanyika mwezi Aprili mjini Beijing, China na Kenya zilisaini makubaliano ya kuiruhusu Kenya kuiuzia China maparachichi, ambayo yanatakiwa kuhifadhiwa katika nyuzijoto 30 chini ya sifuri baada ya kutolewa ngozi, na kusafirishwa katika chombo chenye nyuzijoto 18 chini ya sifuri. Hali hii itawalazimu wakulima wa Kenya kujenga vyumba vya baridi na kununua zana husika. Lakini asilimia 70 ya wakulima wanaopanda maparachichi hawana uwezo huu.

    Bi. Serem amesema, wataalam wa China wamefanya ziara ya pili mwezi Julai nchini Kenya baada ya kuitembelea mwezi Machi, ili kufanya tathmini. Sasa suala wanaofuatilia zaidi ni nzi wa kwenye matunda wanaoweza kuhamia China kutokana na maagizo ya maparachichi mabichi. Hata hivyo ametarajia kuwa pande hizo mbili zitafikia makubaliano haraka.

    Bi. Serem amesema, wakati wa kuadhimisha mwaka wa 56 tangu Kenya na China zianzishe uhusiano wa kibalozi, Kenya inatumai mazao yake ya kilimo ikiwa ni pamoja na kahawa na chai yanaweza kuingia soko la China lenye watu bilioni 1.4.

    Licha ya maparachichi, mwaka huu, Kenya pia imefanikiwa kusaini makualibano na China ya kujenga kituo cha maua ya Kenya mjini Changsha, mkoani Hunan, China, kwenye maonesho ya kwanza ya uchumi na biashara kati ya China na Afrika yaliyofanyika Juni nchini China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako