• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China apongeza kufanyika kwa Maonyesho ya 12 ya China na Kaskazini Mashariki mwa Asia

  (GMT+08:00) 2019-08-23 19:10:33

  Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya pongezi kwa Maonyesho ya 12 ya China na Kaskazini Mashariki mwa Asia yaliyofunguliwa leo mjini Changchun, China.

  Rais Xi amesema, kauli mbiu ya maonyesho hayo ya kuongeza uaminifu na ushirikiano ili kuleta ustawi mzuri zaidi wa kanda ya kaskazini mashariki mwa Asia , imeonesha matumaini ya pamoja ya pande husika ya kupata ustawi na maendeleo ya kikanda. Amesema, hivi sasa, ujenzi wa pamoja wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" unaendelea kutoa nguvu mpya kwenye upanuzi na ongezeko la ushirikiano katika kanda hiyo.

  Rais Xi pia amesema, anatarajia serikali, mashirika na wajumbe wa biashara wataweza kutumia vizuri maonesho hayo kama jukwaa la kufikia makubaliano, kusukuma mbele ushirikiano na kupata mafanikio zaidi ili kujenga mustakabali mzuri zaidi wa kanda hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako