• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wakuu wa Keroche waachiliwa kwa dhamana

  (GMT+08:00) 2019-08-23 20:15:17

  Wakurugenzi wa Keroche Breweries Limited, Afisa Mkuu Mtendaji Tabitha Karanja na mumewe ambaye ndiye mwenyekiti Joseph Karanja wamekanusha mashtaka 10 kuhusu ukwepaji wa ushuru wa Sh14.4 bilioni.

  Wakuu hao wa kiwanda cha kutengeneza pombe na mvinyo mjini Naivasha walikamatwa Alhamisi wiki hii walifikishwa mbele ya hakimu mkuu Francis Andayi.

  Wameachiliwa kwa dhamana ya Sh15 milioni na Sh5 milioni mtawalia.

  Aidha, mahakama imeagiza Keroche ilipe Sh15 milioni katika kipindi cha siku saba la sivyo wakurugenzi watakamatwa isipokuwa Afisa Mkuu Mtendaji.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako