• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wamiliki 163 Tanzanite wabanwa TRA

    (GMT+08:00) 2019-08-23 20:16:16

    Wamiliki 163 wa migodi walioajiri wachimbaji 4,500 wa madini ya Tanzanite katika Mji Mdogo wa Mirerani, Simanjiro mkoani Manyara, wameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwataka kuwalipia kodi ya mapato na ya ufundi wachimbaji hao.

    Meneja wa TRA mkoani Manyara, John Mwigura, alisema kati ya wamiliki hao 163, ni 31 pekee waliopeleka taarifa za wafanyakazi walio nao na namna wanavyofanya shughuli zao migodini.

    Alisema kila wakizungumza na wamiliki hao juu ya kuwalipia kodi ya ajira na tozo ya ufundi kwa wafanyakazi wao, wamekuwa wakitoa sababu tatu kwa TRA ambazo wanadai hawastahili kuzilipa.

    Kwa mujibu wa meneja huyo, sababu ya kwanza wanadai hawajaajiri kwenye migodi, sababu ya pili wameajiri ila hawalipi mishahara na ya tatu hawajapata madini, hivyo hawawezi kulipa chochote.

    Alisema waliwaeleza kuwa wanapaswa kuwapa taarifa za mrejesho wa wanavyofanyia kazi na uzalishaji kila mwezi, lakini hawafanyi, hivyo wanapeleka kwenye ofisi za tume ya madini.

    Alisema endapo wamiliki hao wasipolipia kwa hiyari, watawafikisha mahakamani baada ya kukutana nao Mirerani na kuzungumza nao juu ya malipo hayo kuanzia miaka mitatu iliyopita.

    Alisema wanafanya hayo kupitia sheria ya madini, sheria ya kazi inayowataka wawe na mikataba ya kazi na sheria ya kodi ya mfumo wa kujikadiria kulingana na wafanyakazi walio nao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako