• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Namibia apongeza ziara ya wanaanga wa China

    (GMT+08:00) 2019-08-23 20:24:36

    Rais wa Namibia Hage Geingob jana alipongeza ziara ya wanaanga wa China kwa kupeleka uzoefu wao wa anga ya juu na kuwapa msukumo vijana nchini humo.

    Wanaanga wawili, Liu Yang na Chen Dong, wamefanya ziara ikulu jana ambako rais aliwakaribisgha kwa mikono miwili. Geingob amesema ziara ya wanaanga hao ni muhimu wakati ambao mataifa mawili yanapata kupeana uzoefu wa anga ya juu. Hata hivyo rais amesema bahati mbaya nchi yake haiwezi kumudu kurusha chombo cha anga ya juu, lakini kupata uzoefu wa nchi rafiki kama China, kwao wao inatosha kabisa.

    Naye naibu waziri wa elimu ya juu, mafunzo na uvumbuzi Becky Ndoze-Ojo amemwelezea rais jinsi wageni wao walivyoshirikiana na wanafunzi wa mkoa wa Erongo na Windhoek wakati wa ziara yao ya siku tano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako