• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuongeza ushuru kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 75

  (GMT+08:00) 2019-08-23 20:32:21

  Tume ya Ushuru wa Forodha ya Baraza la Serikali la China imetangaza kuwa China itaongeza ushuru kwa asilimia 10 au 5 kwa bidhaa tofauti zilizozalishwa nchini Marekani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 75, ikiwa ni jibu dhidi ya uamuzi wa Marekani wa kuongeza ushuru kwa asilimia 10 dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 300.

  Hatua hiyo itachukuliwa kwa sehemu mbili kuanzia saa 6:01 mchana ya tarehe mosi, Septemba, na saa 6:01 mchana ya tarehe 15, Disemba kwa saa za hapa Beijing ambayo itatekelezwa sambamba na utekelezaji wa sehemu mbili za upande wa Marekani kwa saa za huko.

  China imerejea msimamo wake tena kuwa ushirikiano ni chaguo pekee sahihi kwa nchi mbili za China na Marekani, na ni kupitia ushirikiano wa kunufaishana tu ndipo siku za baadaye za nchi hizo mbili zitakuwa nzuri.

  Wakati huohuo, China itaendelea kutoza nyongeza ya ushuru kwa asilimia 25 au asilimia 5 dhidi ya magari yaliyotengenezwa nchini Marekani na vipuri vyake kuanzia saa 6:01 ya tarehe 15, Disemba kwa saa za Beijing.

  Ili kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na marais wa China na Marekani nchini Argentina, kuanzia tarehe mosi, Januari mwaka huu, China ilisitisha kutoza nyongeza ya ushuru kwa magari yaliyotengenezwa nchini Marekani na vipuri vyake kwa miezi mitatu, na ilisitisha tena tarehe mosi, Aprili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako