• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Makala yasema mabavu ya bunduki nchini Marekani yanakanyaga haki za binadamu

  (GMT+08:00) 2019-08-25 20:20:13

  Taasisi ya Utafiti wa Haki za Binadamu ya China imetoa makala ya kufichua tatizo sugu ambalo halijapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu la mabavu ya kutumia bunduki nchini Marekani, ambayo imesema yamekiuka vibaya haki za binadamu.

  Ikikumbusha kuwa mashambulizi mengi ya bunduki yaliyosababisha vifo vya watu yametokea hivi karibuni nchini Marekani, makala hiyo inasema hayo yameonyesha kwa mara nyingine tena matokeo mabaya ya kuenea kwa bunduki na pia msukosuko mbaya wa mifumo ya kisiasa na kijamii nchini humo, pamoja na unafiki wake kuhusu haki za binadamu.

  Makala hiyo pia imesema mashambulizi ya bunduki nchini Marekani yamesababisha vifo na majeruhi wengi, na ni tishio kubwa dhidi ya usalama wa umma. Makala imeongeza kuwa mabavu ya kutumia bunduki yanakanyaga vibaya haki za binadamu, hasa kukiuka moja kwa moja haki ya uhai ya raia wa Marekani, suala ambalo linahusiana na mifumo maalumu ya kijamii na kisiasa ya nchi hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako