• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la utawala la Sudan lamfuta kazi gavana wa Jimbo la Bahari Nyekundu kutokana na mapigano ya kikabila

  (GMT+08:00) 2019-08-26 08:25:08

  Baraza la utawala la Sudan lililoundwa karibuni Jumapili limetangaza kumfuta kazi gavana wa Jimbo la Bahari Nyekundu mashariki mwa nchi hiyo, baada ya kutokea kwa mapigano ya kikabila jimboni humo.

  Baraza hilo pia limemwondoa kazini mkurugenzi wa idara ya usalama wa jimbo hilo, na kurejesha tena hali ya dharura katika jimbo hilo na kuamuru uchunguzi ufanyike kuhusu matukio hayo.

  Mapema siku hiyo, polisi wa Sudan walitangaza kwamba watu 17 waliuawa katika mapigano kati ya makabila mawili katika mji wa Port Sudan, mji mkuu wa Jimbo la Bahari Nyekundu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako