• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Klabu bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, Simba, KMC zatolewa, Yanga na Azam zapeta

  (GMT+08:00) 2019-08-26 08:28:40

  Mwishoni mwa wikiendi kulipigwa michezo kadhaa ya klabu bingwa Afrika ambapo wawakilishi wa Tanzania Yanga waliifurumusha wacheza Makhirikhiri wa Botswana, Township Rollers kwa goli 1-0 jijini Gaborone nchini humo. Huku watani wao wa jadi Wekundu wa Msimbazi Simba wakiwa nyumbani uwanja wa taifa jana wameondolewa katika michuano hiyo baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Wamakonde wa Msumbiji US Songo. US Songo imepata faida ya goli la ugenini.

  Katika kombe la shirikisho, KMC imeshindwa kutumia vyema uwanja wake wa nyumbani na kukubali kupigwa 2-1 na kufungasha virago baada ya kupoteza mchezo dhidi ya AS Kigali ya Rwanda. Azam FC imekataa uteja kwa mara ya pili baada ya kuwachapa Fasil Kenema 3-2.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako