• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Watu wanane wauawa katika mpaka wa Kenya na Ethiopia kutokana na wizi wa ng'ombe

  (GMT+08:00) 2019-08-26 08:50:14

  Polisi nchini Kenya jana walithibitisha kuwa watu wanane wameuawa na wengine 9 kujeruhiwa katika matukio ya wizi wa ng'ombe kwenye kaunti ya Marsabit karibu na mpaka kati ya Ethiopia na Kenya.

  Mkuu wa polisi wa kaunti hiyo Bw. Steve Oloo amesema, mashambulizi ya kutumia silaha yalitokea kwenye vijiji vya Forole na Sabareh kwenye mpaka kati ya Ethiopia na Kenya, na washambuliaji hao walitoroka na kuiba mifugo ambayo idadi yake haijulikani.

  Bw. Oloo pia amesema, wamepeleka polisi zaidi katika eneo hilo ili kudhibiti hali ya usalama, na polisi hao pia watafanya uchunguzi kuhusu mashambulizi hayo mawili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako