• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatangaza kuanzisha maeneo sita ya majaribio ya biashara huria

  (GMT+08:00) 2019-08-26 18:52:48

  China leo imetangaza mpango wa kuanzisha maeneo sita ya majaribio ya biashara huria, ambayo ni hatua ya kimkakati ya kuhimiza mageuzi na kufungua mlango katika zama mpya.

  Kwa mujibu wa mpango huo, maeneo hayo sita yataanzishwa kwenye mikoa sita ya China, ikiwa ni pamoja na Shandong, Jiangsu, Guangxi, Hebei, Yunnan na Heilongjiang. Mpango huo unasema kuanzishwa kwa maeneo hayo sita ya majaribio ya biashara huria ni uamuzi muhimu uliotolewa na Kamati kuu la Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la serikali ya China, pia ni hatua ya kimkakati ya kuhimiza mageuzi na kufungua mlango katika zama mpya.

  Hadi sasa idadi ya maeneo ya majaribio ya biashara huria ya China imefikia 18, ambayo yakiwa ni watangulizi wa mageuzi na kufungua mlango, yatafanya majaribio juu ya mifumo mipya katika usimamizi wa uwekezaji nje, urahisi wa biashara na mageuzi ya kazi za serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako