• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yachukua msimamo wa kimantiki kukabiliana na umwamba wa kibiashara wa Marekani

    (GMT+08:00) 2019-08-26 18:55:55

    Jumamosi iliyopita Marekani ilitangaza kuongeza tena ushuru wa asilimia 5 dhidi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 550. China inapinga kithabiti hatua hii, na Wizara ya mambo ya nje ya China imetangaza kuwa endapo hatua hizo zitatekelezwa, China itaendelea kuchukua hatua ili kulinda maslahi yake halali.

    Marekani inaongeza ushuru kadiri inavyotaka, lakini haiwaruhusu wenzi wake wa kibiashara kuchukua hatua mwafaka ya kujibu, kitendo ambacho kimefafanua wazo lake wa umwamba wa kimarekani. Lakini China itachukua hatua zinazotakiwa ili kukabiliana kwa msimamo wa kimantiki.

    Hivi sasa utaratibu wa pande nyingi na kufanya ushirikiano wa pande nyingi ni mwelekeo usiozuilika. Ndiyo maana, vita ya biashara iliyoanzishwa na baadhi ya wamarekani kote duniani imepuuzwa na wenzi wake wengi wa biashara.

    Kwa mfano, India imeanza kutoza ushuru dhidi ya bidhaa za aina 28 za Marekani kuanzia Juni 16. Mwezi Julai, Mjumbe maalumu wa biashara wa Umoja wa Ulaya Cecilia Malmstrom alisema, endapo Marekani itaongeza ushuru kwa magari na vipuri vinavyohusika vinavyoagizwa kutoka Umoja huo, utaijibu kwa kutoza ushuru kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya Euro bilioni 35. Naye rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ameeleza kuwa, ni lazima kuchukua hatua inayosaidia kupunguza uhusiano wa mashaka, ili kuzuia vita hii ya biashara inayoenea duniani. Mwenyekiti wa Baraza la Ulaya Donald Tusk ameonya kuwa, uhusiano wa mashaka wa kibiashara kati ya Marekani na nchi nyingine unaozidi kuongezeka utaweza kuufanya uchumi wa dunia kudidimia.

    Kwa upande mwingine, China inachukua msimamo wa kimantiki ambao unazingatia maslahi ya pamoja, ambao unachukuliwa na jumuiya ya kimataifa kama ni njia mwafaka ya kukabiliana na umwamba wa kibiashara wa Marekani.

    China siku zote inachukua msimamo wazi dhidi ya vita ya biashara: haipendi kufanya vita ya biashara, lakini haina hofu ya kufanya hivyo, na itafanya kama ikilazimika. China inapenda kutatua masuala juu ya msingi wenye usawa na kuheshimiana, lakini kamwe haitasalimu amri mbele ya masuala muhimu, na mashinikizo makubwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako