• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China apongeza kufunguliwa kwa maonesho ya kimataifa ya Smart China ya mwaka 2019

    (GMT+08:00) 2019-08-26 19:08:44

    Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya pongezi kwa maonesho ya kimataifa ya Smart China ya mwaka 2019 yaliyofunguliwa leo huko Chongqing.

    Rais Xi amesema, hivi sasa teknolijia ya mawasiliano ya habari ya kisasa inaendelea siku hadi siku ikiwemo mtandao wa Internet, data kubwa na akili bandia, huku duru mpya ya mapinduzi ya sayansi na teknolojia na mabadiliko ya shughuli hizo zikiendelea kupiga hatua. Ukuaji wa kasi wa shughuli za akili bandia zitaleta athari kubwa na za kina kwa maendeleo ya uchumi, jamii na usimamizi wa dunia.

    Amesisitiza kuwa China inatilia maanani shughuli za teknolojia ya akili bandia na kuhimiza uunganishaji wa kina wa uchumi wa kidigitiali na uchumi halisi. Pia amesema China inapenda kushirikiana na jumuiya ya kimataifa kufungua zama ya akili bandia na kunufaishwa na maendeleo yanayoletwa na teknolojia hiyo.

    Habari zinasema, naibu waziri mkuu wa China Bw. Liu He amehudhuria maonesho hayo, akisema China inawakaribisha wawekezaji wa nchi mbalimbali duniani ikiwemo Marekani kuwekeza na kuanzisha shughuli nchini China, na itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji, kulinda hakimiliki za ujuzi huku ikisukuma mbele maendeleo ya teknolojia ya akili bandia katika sharti la ufunguaji mlango wazi, kupinga vizuizi vya teknolojia na ulinzi wa kiuchumi na kulinda ukamilifu wa mnyororo wa shughuli hiyo.

    Ameongeza kuwa China inapenda kuwa na msimamo wenye utulivu kutatua masuala kupitia ushirikiano na mazungumzo, na kupinga kithabiti kupamba moto kwa vita ya kibiashara. Kwa kuwa inaona kuwa vita hiyo haitainufaisha China wala Marekani, na haina maslahi ya watu wa dunia nzima.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako