• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa nane wa kamati ya 13 ya wajumbe wa kudumu ya baraza la mashauriano ya kisiasa la China wafunguliwa

    (GMT+08:00) 2019-08-26 19:50:13

    Mkutano wa nane wa kamati ya 13 ya wajumbe wa kudumu ya baraza la mashauriano ya kisiasa la China umefunguliwa hapa Beijing, ukijadili kuhusu namna ya kutekeleza elimu inayoridhisha watu.

    Mjumbe wa ofisi ya siasa ya kamati kuu ya chama cha kikomunisti cha China ambaye pia ni naibu waziri mkuu wa China Bi. Sun Chunlan amehudhuria mkutano na kutoa hotuba. Amesema tangu mkutano mkuu wa 19 wa wajumbe wa chama cha kikomunisti cha China ulipofanyika, China inaendelea kuongeza ufadhili wa elimu na kuimarisha mafunzo kwa timu za walimu.

    Amesema ili kufanya elimu iwaridhishe wananchi, pande mbalimbali zinatakiwa kufanya juhudi za pamoja kuboresha mazingira, ili kutekeleza kihalisi maamuzi na mipango ya kamati kuu ya chama na baraza la serikali kuhusu kazi za elimu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako