• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa 8 wa kongamano la washauri mabingwa wa China na Afrika wafanyika hapa Beijing

  (GMT+08:00) 2019-08-26 20:00:06

  Mkutano wa 8 wa kongamano la washauri mabingwa wa China na Afrika umefanyika hapa Beijing, na kuhudhuriwa na watu karibu 400 wakiwemo mabalozi wa nchi 45 za Afrika nchini China, maofisa wa serikali, wasomi na wanahabari wa nchi 51 za Afrika, pamoja na wajumbe wa China.

  Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Chen Xiaodong akihutubia ufunguzi wa mkutano huo amesema, China inapenda kufanya juhudi pamoja na Afrika, kushikilia mwelekeo wa kimsingi wa kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya China na Afrika uliotolewa kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la Ushirikiao kati ya China na Afrika FOCAC, na kutekeleza maoni ya kimkakati na makubaliano yaliyofikiwa na viongozi wa pande hizo mbili kwenye mkutano huo. Amesisitiza kuwa China itaendelea kuunga mkono nchi za Afrika kutoa mchango zaidi katika mambo ya kimataifa.

  Balozi wa Umoja wa Afrika nchini China Rahamtalla Mohamed Osman amesema, makubaliano mengi yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa Beijing wa FOCAC yanalingana pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na "Ajenda ya Mwaka 2063" ya Umoja wa Afrika, na yatahimiza mafungamano ya utamaduni na uchumi kati ya pande hizo mbili, kuinua kiwango cha utawala wa kimataifa, kutoa nafasi sawa kwa watu wote, na kuleta maendeleo ya pamoja. Ameongeza kuwa, ushirikiano kati ya Afrika na China katika sekta nyingi utaleta mafanikio halisi na kunufaisha bara la Afrika.

  Profesa wa taasisi ya uhusiano wa kimataifa ya Chuo Kikuu cha Umma cha China Wang Yiwei amesema, China na Afrika ni wenzi wa kiasili katika ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na jumuiya yenye hatma ya pamoja. Anaona kuwa ujenzi wa jumuiya hiyo unapaswa kutekelezwa kwa hatua tatu, kwanza ni kutafuta na kupata njia inayofaa ya kuendeleza uchumi haswa sekta ya viwanda, pili ni kufanya mawasiliano na ushirikiano katika pande mbalimbali, na tatu ni kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya nchi za Afrika, kati ya Afrika na China, kati ya nchi zinazoendelea, na kati ya binadamu wote.

  Mshauri wa mkuu wa Chuo Kikuu cha Dakar cha Senegal Amadou Falilou Ndiaye amesema, ubora wa uhusiano kati ya China na Afrika unatokana na kuheshimiana, usawa, uaminifu na mafanikio ya pamoja, na ushirikiano umeimarisha uwezo wa pande hizo zote katika sekta mbalimbali, ikiwa ni pamoja na biashara, kilimo, viwanda, teknolojia na miundombinu.

  Kongamano la washauri mabingwa wa China na Afrika lilianzishwa mwaka 2011 na taasisi ya utafiti wa mambo ya Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha mkoa wa Zhejiang, kwa madhumuni ya kuhimiza mawasiliano na maelewano kati ya pande hizo mbili, na hufanyika kwa zamu nchini China na barani Afrika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako