Ofisa mkuu wa Benki hiyo Bw. Kariuki Ngari amesema mjini Nairobi kuwa kutokana na kuimarika kwa uwekezaji na biashara kati ya China na Kenya, wateja wa benki hiyo wanaangalia njia za kuweza kufanya malipo ya kuvuka mpaka. Amesema kutokana na mahitaji ya wateja, wanaweza kuunganisha majukwaa ya malipo kwa njia ya mtandao kama vile Alipay na WeChat, ili kurahisisha malipo kwenye biashara kati ya China na Kenya.
Bw. Ngari amesema jumuiya ya wafanyabiashara wa China kwa sasa inatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa Kenya, na Benki ya Standard Chartered imeanzisha dawati la China kwenye matawi yake ili kuhudumia wateja wake wa China.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |