• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi na taasisi za Afrika zahimizwa kujenga uchumi unaohimili mabadiliko ya tabianchi

    (GMT+08:00) 2019-08-27 08:00:04

    Nchi na taasisi za Afrika zimehimizwa kuendeleza juhudi za pamoja kuelekea kujenga uchumi unaoweza kuhimiza mabadiliko ya tabianchi kote barani humo.

    Wito huo umetolewa na Umoja wa Afrika Jumatatu wakati bara la Afrika linakuwa mwenyeji wa Mkutano wa ngazi ya juu kuhusu mabadiliko ya tabianchi utakaofanyika wiki hii mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo umeandaliwa kwa pamoja na Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Kamisheni ya Uchumi wa Afrika ya Umoja wa Mataifa ECA, Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB, na Shirika linalojihusisha na masuala ya hali ya hewa barani Afrika PACJA.

    Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika inasema, Mkutano kuhusu mabadiliko ya tabianchi na maendeleo barani Afrika CCDA utakaofanyika kwa siku tatu kuanzia Agosti 28, ni kikao maalumu cha maandalizi ya Afrika kwa ajili ya Mkutano wa kilele wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi utakaoitishwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 23 mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako