• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Zambia yasema iko kwenye mwelekeo sahihi wa kutekeleza hatua za kuimarisha masuala ya kifedha

  (GMT+08:00) 2019-08-27 08:09:56

  Serikali ya Zambia imesema kuwa imepata maendeleo katika kutekeleza hatua za kuimarisha masuala ya fedha.

  Waziri wa Fedha nchini humo Bwalya Ng'andu amesema, serikali itaendelea kushikilia utekelezaji sahihi wa hatua hizo, kudhibiti kikamilifu deni la taifa, na kwamba mpango wa utulivu wa uchumi umeendelea katika mwelekeo sahihi kwa kuendana na matarajio ya ustawi na ukuaji wa nchi.

  Wiki iliyopita, Benki Kuu ya Zambia ilisema ukosefu wa utekelezaji sahihi wa hatua za kuimarisha masuala ya kifedha kunaathiri vibaya uchumi wa nchi hiyo, kama inavyodhihirika kutokana na shinikizo katika maeneo makuu ya kiuchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako