• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ofisa asema uvuvi haramu nchini Tanzania unakaribia kudhibitiwa

  (GMT+08:00) 2019-08-27 08:10:21

  Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi nchini Tanzania Bw. Abdallah Ulega amesema, uvuvi haramu ambao ulienea sana nchini humo kwa sasa umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

  Akizungumza katika soko la samaki lililoko Kunduchi jijini Dar es Salaam, waziri huyo amesema serikali imefanikiwa kudhibiti uvuvi wa kutumia baruti katika bahari ya Hindi na maziwa makuu nchini humo. Pia amesema, kwa mwaka huu, hakuna ripoti zozote zilizopokelewa zinazoonyesha matukio ya uvuvi kwa kutumia baruti.

  Bw. Ulega amesema, ushirikiano mzuri kati ya mamlaka husika na wavuvi ni moja ya sababu za mafanikio yaliyopatikana katika mapambano dhidi ya uvuvi haramu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako