• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika watoa mafunzo kwa maofisa ya kijeshi ili kuimarisha usalama Somalia

  (GMT+08:00) 2019-08-27 08:38:04

  Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kimekamilisha mafunzo kwa maofisia wa kijeshi kutoka nchi sita za kikanda ili kusaidia kuimarisha utulivu nchini Somalia.

  Umoja wa Afrika pia umewahimiza maofisa wa kijeshi kutoka Burundi, Ethiopia, Kenya, Sierra Leone, Uganda na Zimbabwe kufanya juhudi za kutekeleza majukumu yao katika operesheni za AMISOM.

  Katika mafunzo hayo ya siku tano, maofisa hao walifahamishwa majukumu yao na kupewa ujuzi na ufundi utakaowawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi katika kuisaidia AMISOM kutekeleza majukumu yake.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako