Idadi ya watoto wasiosajiliwa walipozaliwa nchini Nigeria imefikia milioni 19. Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema hiyo inatokana na mfumo dhaifu wa usajili wa uzazi, ikiwa ni pamoja na mpango mbaya, ukosefu wa uwezo wa kuanzisha takwimu husika za afya ya umma na makadirio na mpango wa idadi ya watu kote nchini. UNICEF imesema watoto wasiosajiliwa wanatoka familia zenye hali duni ya kiuchumi, kielimu na katika sehemu za vijijini.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |