• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Iran wakutana

  (GMT+08:00) 2019-08-27 09:09:45

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na mwenzake wa Iran Mohammad Javad Zarif jana hapa Beijing.

  Bw. Wang Yi amesema, China na Iran zikiwa ni wenzi wa kimkakati wa pande zote, zinapaswa kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kushirikiana na nchi nyingine kulinda mfumo wa pande nyingi, kushikilia kanuni ya kimsingi ya mahusiano ya kimataifa, na kulinda maslahi halali ya nchi mbalimbali. Pia amesema, China inaunga mkono juhudi zote zinazosaidia kulinda makubaliano ya nyuklia ya Iran JCPOA, na inapenda makubaliano hayo yaendelee kutekelezwa, na kufanya kazi ya kiujenzi kwa ajili ya kupunguza hali ya wasiwasi ya kanda ya ghuba.

  Bw. Zarif amesema, Iran inapenda kushirikiana na China katika kuimarisha ushirikiano katika sekta za siasa, uchumi, sayansi na teknolojia, utamaduni na kujenga kwa pamoja "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na kuhimiza uhusiano kati ya nchi hizo mbili kuendelezwa zaidi. Pia amemwarifu Bw. Wang Yi kuhusu matokeo ya ziara yake barani Ulaya kuhusu kulinda makubaliano ya nyuklia ya Iran, na kusisitiza kuwa Iran itaendelea na juhudi za kutatua masuala husika kwa njia ya mazungumzo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako