• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yahimiza kuunga mkono serikali ya Sudan kudumisha usalama katika sehemu ya Darfur

  (GMT+08:00) 2019-08-27 09:40:29

  Naibu balozi wa kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao ameihimiza jumuiya ya kimataifa kuunga mkono serikali ya Sudan kubeba jukumu kuu la kudumisha usalama katika sehemu ya Darfur nchini humo.

  Akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Tume ya pamoja ya Umoja huo na Umoja wa Afrika katika Darfur UNAMID, Bw. Wu amesema jumuiya ya kimataifa inapaswa kuisaidia serikali ya Sudan kuimarisha uwezo wake wa usalama na utawala, na kuhakikisha jukumu la kulinda usalama katika Darfur linakabidhiwa kwa vikosi vya usalama vya Sudan kwa utulivu.

  Ameongeza kuwa China inakubali mpango wa kuondoa kikosi hicho itakapofika tarehe 30 June mwakani, kufuatia azimio namba 2429 lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

  Tarehe 27 Juni, Umoja wa Mataifa uliamua kusimamisha mpango huo kutokana na mkwaruzano kati ya Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan TMC na muungano wa upinzani. Kwenye mkutano uliofanyika jana, Umoja huo umesema kutokana na kuundwa kwa serikali mpya ya pamoja nchini Sudan, utafikiria tena mpango huo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako