• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mapigano ya kikabila yasababisha vifo vya watu 37 mashariki mwa Sudan

  (GMT+08:00) 2019-08-27 18:16:16

  Mapigano ya kikabila yaliyotokea kuanzia tarehe 21 katika mji wa Port-Sudan wa jimbo la Red Sea nchini Sudan, yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 37 na wengine zaidi ya 200 kujeruhiwa.

  Polisi ya Sudan hivi karibuni imetoa taarifa ikisema, pande mbili za mapigano za kabila la Bani Amer na kabila la Al-Nuba, zimekuwa na uhasama wa muda mrefu, na polisi wameongeza nguvu katika sehemu za mapigano ili kudhibiti hali ya huko. Chanzo cha mapigano hayo bado hakijajulikana.

  Baada ya mapigano hayo kutokea, baraza la mamlaka ya pamoja la Sudan limetangaza hali ya dharura katika jimbo la Red Sea, na kuamuru kuundwa tume ya uchunguzi kuhusu mapigano hayo. Kutokana na kushindwa kutatua mapigano hayo, kaimu gavana wa jimbo hilo na mkurugenzi wa idara ya usalama wamefukuzwa kazi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako