• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima kutoka Kaskazini mwa Bonde la Ufa sasa wakodolewa macho na hasara kubwa

    (GMT+08:00) 2019-08-27 19:21:31
    Wakulima kutoka Kaskazini mwa Bonde la Ufa sasa wanakodolewa macho na hasara kubwa baada ya mahindi yaliyoagizwa na serikali kutoka Uganda na Tanzania kujaa sokoni.

    Kampuni za kibinafsi za kusaga mahindi nazo hazijaachwa nyuma, kwa kuwa zimekuwa zikinunua mazao hayo kutoka mataifa hayo mawili kwa bei ya chini ya Sh2,400 kwa kila gunia.

    Serikali nayo imekosa kutoa magunia milioni 2 ya mahindi ya bei nafuu jinsi ilivyoahidi na kuchangia kampuni hizo kukimbilia mahindi kutoka nje huku wakulima wakiumia kwa kukosa soko la kuuza mazao hayo.

    "Wakulima wa mahindi wanakodolewa macho na hasara kubwa kutokana na kushuka kwa bei ya mahindi huku mazao haya yakiletwa kwa wingi kutoka Tanzania na Uganda," akasema mmoja wa wamiliki wa kampuni za kusaga mahindi Jackson Too.

    Mwenyekiti wa Bodi ya Kuhifadhi Chakula(SFR) Dkt Noah Wekesa alisema Bodi ya Kitaifa ya Nafaka na Mazao(NCPB) bado haijatoa maguni milioni 2 ya mahindi ya bei nafuu ambayo yatauzwa kwa Sh2, 700 kwa kila gunia la kilo 90 kutokana na ukosefu wa fedha.

    Dkt Wekesa alithibitisha kwamba magunia kadha ya mahindi bado yataagizwa kutoka mataifa wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) ili kuwawezesha Wakenya kumudu bei ya unga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako