• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda yazindua safari za shirika lake la taifa la ndege

  (GMT+08:00) 2019-08-27 19:38:24

  Shirika la ndege la Uganda limeanzisha safari za kibiashara leo na safari yake ya kwanza ni kwenda Nairobi.

  Akizindua safari ya kwanza kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe, waziri mkuu wa Uganda Bw. Ruhakana Rugunda amesema huo ni wakati wa furaha, hasa kutokana na kuwa shirika hilo la ndege lilikufa mwaka 2001.

  Akisoma hotuba kwa niaba ya Rais Museveni, Bw. Rugunda amesema kila mwaka waganda wanatumia dola milioni 450 katika nchi nyingi kusafiri nje ya nchi. Amesema licha ya kupata usumbufu, waganda pia wamekuwa wakilipia gharama kubwa kutokana na kutokuwa na shirika lao la ndege.

  Shirika hilo kwanza litakuwa na safari za kwenda Nairobi, Mogadishu, Juba, na Dar es salaam, halafu litafuatia na safari za kwenda Mombasa, Kilimanjaro na Bujumbura.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako