• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa nane wa kongamono la jopo la washauri bingwa kati ya China na Afrika wafanyika Beijing

  (GMT+08:00) 2019-08-27 19:44:57

  Mkutano wa nane wa kongamono la jopo la washauri bingwa kati ya China na Afrika unaofanyika kwa siku mbili umefunguliwa jana mjini Beijing. Washiriki wa mkutano huo wanakongamana kujadili utekelezaji wa matokeo ya mkutano wa FOCAC wa Beijing na kutoa mapendekezo kwa ajili ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya China na Afrika.

  Msaidizi wa waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Chen Xiaodong, amesema China na Afrika zinapaswa kudumisha mawasiliano ya ngazi na sekta mbalimbali, kuimarisha uoanishaji kati ya ujenzi wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na Ajenda ya mwaka 2063 kwa Afrika pamoja na mikakati ya maendeleo ya nchi za Afrika. Pia amesema pande zote mbili zinatakiwa kulinda maslahi ya pamoja ya nchi zinazoendelea.

  Mjumbe wa Umoja wa Afrika nchini China Bw. Rahmat Allah Mohamed Osman amesema "Hatua kuu nane" za ushirikiano kati ya China na Afrika zilizotolewa na mkutano wa FOCAC wa Beijing zinaendana na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na lengo la Ajenda ya mwaka 2063 kwa Afrika, ambazo zitahimiza maendeleo ya pande zote mbili, na kuhimiza mafungamano ya utamaduni na uchumi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako