• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yasema hakuna anayeruhusiwa kuingilia mambo ya Hong Kong kwa kutumia Taarifa ya pamoja kati ya China na Uingereza

  (GMT+08:00) 2019-08-27 19:52:11

  Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema nchi yoyote au kundi lolote haliruhusiwi kuingilia mambo ya Hong Kong kwa kutumia Taarifa ya pamoja kati ya China na Uingereza.

  Bw. Geng amesema China inapinga vikali taarifa iliyotolewa na viongozi wanaoshiriki kwenye mkutano wa kilele wa kundi la G7, ambayo inatoa maoni yasiyowajibika juu ya mambo ya Hong Kong.

  Amesisitiza kuwa mambo ya Hong Kong ni mambo ya ndani ya China, serikali yoyote, shirika lolote na mtu yeyote haruhusiwi kuingilia. Nchi wanachama wa kundi hilo zisiwe tena na mawazo mabaya juu ya mambo hayo. Kwa mujibu wa sheria ya kimataifa na kanuni za kimsingi za uhusiano wa kimataifa, nchi yoyote na shirika lolote haliruhusiwi kuingilia mambo ya Hong Kong kwa kutumia Taarifa ya pamoja kati ya China na Uingereza.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako