• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkoa wa Jiangsu wa China waanzisha vituo saba vya sheria ili kuhudumia kampuni za China kuwekeza nchi za nje

    (GMT+08:00) 2019-08-27 20:00:43

    Naibu kiongozi wa Shirika la Wanasheria wa Mkoa wa Jiangsu Bw. Wang Xiaoqing amesema hadi sasa mkoa wa Jiangsu umeanzisha vituo saba vya huduma za kisheria nchini Cambodia, Umoja wa Falme za Kiarabu UAE, Russia, Brazil, Angola, Ethiopia, Indonesia na kuandaa ofisi za utoaji wa huduma za kisheria nje ya nchi kwenye maeneo makuu ya Ukanda Mmoja, Njia Moja ili kuzihudumia kampuni za China kuanzisha biashara katika nchi za nje.

    Bw. Wang amesema hayo kwenye mkutano wa kawaida na waandishi wa habari wa Shirika la Wanasheria la kitaifa la China, akiongeza kuwa malengo ya vituo hivyo ni kukusanya rasilimali za huduma za kisheria, kuchunguza uanzishaji wa mfumo wa kukabiliana na msukosuko mkubwa wa nje, na kuwapa msaada wa kisheria wenye ukomo kwenye misukisuko mikubwa ya kisheria na kesi zinazohusu kampuni za nje na wananchi, na kuimarisha uzuiaji na onyo la mapema la hatari za kisheria, hatari za sera na migongano ya kidini, na hatari za ajira kwa wafanyakazi zinazosababishwa na tofauti za kisheria katika biashara za nje.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako