• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi za China nchini Uganda na Kenya zafanya sherehe ya kuwaaga wanafunzi waliopata udhamini wa serikali ya China

  (GMT+08:00) 2019-08-28 08:06:50

  Wanafunzi 111 wa Uganda waliopata udhamini kutoka serikali ya China watakuja China hivi karibuni kuanza masomo yao katika vyuo vikuu mbalimbali.

  Akiongea kwenye sherehe ya kuwaaga wanafunzi hao, Balozi wa China nchini Uganda Zheng Zhuqiang, amesema hii ni idadi kubwa ya wanafunzi waliopata udhamini na kwamba imeongezeka kwa asilimia 59 ikilinganishwa na mwaka jana. Amefafanua kuwa mbali na udhamini wa serikali, kila mwaka karibu wanafunzi 500 wa nchi hiyo wanakuja China kwenye mafunzo ya muda mfupi.

  Nako nchini Kenya, ubalozi wa China nchini humo jana pia ulifanya sherehe ya kuwaaga wanafunzi zaidi ya 200 waliobahatika kupata udhamini wa masomo kutoka China. Wanafunzi hao wanaotarajiwa kuja China baadaye wiki hii, na kuchukuliwa kwenye taasisi za elimu ya juu watasomea kozi mbalimbali zikiwemo uhandisi, matibabu, sheria na lugha ya Kichina katika ngazi za shahada ya kwanza na pili.

  Kwa mengi zaidi tunaungana na mwandishi wetu Jacob Mogoa akiwa mjini Nairobi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako