• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afrika Kusini kuendelea kushiriki kwenye ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi

  (GMT+08:00) 2019-08-28 08:25:18

  Mwakilishi wa kudumu wa Afrika Kusini katika Umoja wa Mataifa Balozi Jerry Matjila amesema nchi yake itaendelea kushiriki kwenye ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na ugaidi.

  Akizungumza kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu "Matishio ya Ugaidi kwa Amani na Usalama wa Kimataifa", Balozi Matjila amesisitiza dhamira ya Afrika Kusini ya kupambana na ugaidi kwa pande zote, na pia kuondoa vyanzo vya ugaidi kwa mujibu wa sheria ya kimataifa.

  Amesema hakuna nchi yoyote duniani inayoweza kukabiliana na ugaidi peke yake, na nafasi unayochukua Umoja wa Mataifa katika kuratibu na kuhimiza juhudi za kimataifa za kupambana na ugaidi na kutoa misaada kwa nchi wanachama zinazoihitaji, ina umuhimu mkubwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako