• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TENISI: Serena adhihirisha umwamba wake kwa Sharapova

  (GMT+08:00) 2019-08-28 08:42:49

  Bingwa mara nyingi wa tenisi duniani Serena Williams amerudi kivingine na kudhihirisha umwamba wake mbele ya Maria Sharapova katika michuano ya wazi ya tenisi ya Marekani, mchezo uliochezwa uwanja wa Arthur Ashe.

  Mambo mengi yamebadilika tangu wacheza tenisi hao wawili walipokutana mara ya mwisho katika michuano hii Januari 2016, huku Sharapova akiendelea kuwa mpinzani halisi wa Serena.

  Ushindi wa seti 6-1, 6-1 ulihitaji dakika 59 tu kwa Serena kumshinda Sharapova. Kocha wa Serena, Patrick Mouratoglou amesema ushindi wa Serena, umetokana na kuweka juhudi katika mazoezi na kuyafanyia kazi makosa yaliyojitokeza katika michuano ya mwisho ya tenisi ambapo alishindwa kufua dafu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako