• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yasifu makampuni ya China kwa kuzisaidia jamii za kienyeji

    (GMT+08:00) 2019-08-28 09:37:22

    Juhudi za makampuni ya China kuzisaidia jamii za Kenya zimeongeza ajira, kuleta mafunzo ya ufundi stadi na kupunguza umaskini kwa raia wa nchi hiyo.

    Hayo yamesemwa na naibu waziri wa mambo ya nje ya Kenya Ababu Namwamba wakati akihutubia kwenye uzinduzi wa ripoti ya majukumu ya kijamii ya mwaka 2018-2019 iliyotolewa na Shirikisho la Uchumi na Biashara la Kenya na China. Amesema vitendo vya makampuni ya China vya kutekeleza wajibu wa kijamii ni mfano wa ustawi wa pamoja, ambapo watu wa Kenya na China wote wanafaidika na uhusiano huu.

    Naye Balozi wa China nchini Kenya Wu Peng amesema nchini Kenya kuna makampuni zaidi ya 400 ya China, ambayo yameleta ajira laki 1.3 kwa Kenya. Ameongeza kuwa, mwaka jana, makampuni ya China yalitoa zaidi ya dola milioni 75 za kimarekani kuzisaidia jamii za Kenya kuboresha elimu, na kuinua kiwango cha maisha kwa kujenga barabara na miundombinu ya maji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako