• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampeni za uchaguzi wa Seneti nchini Rwanda zazinduliwa

  (GMT+08:00) 2019-08-28 09:38:17

  Kampeni za uchaguzi wa baraza la seneti la Rwanda zimezinduliwa rasmi jana. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi ya Rwanda Kalisa Mbanda amesema wagombea 63 wa viti vya useneta wameanza kampeni zao kwenye majimbo na taasisi wanazoziwakilisha kwa mujibu wa mpango wa tume hiyo.

  Ameongeza kuwa, kampeni hizo zitaendelea mpaka tarehe 15 Septemba, na matokeo ya uchaguzi yanatarajiwa kutangazwa tarehe 30, Septemba.

  Baraza la seneti la Rwanda lina viti 26. Kwenye uchaguzi wa seneti uliopangwa kufanyika tarehe 16 hadi 18 Septemba, viti 12 kati ya hivyo vitachaguliwa na kamati maalumu kwa mujibu wa kanuni za usimamizi, viwili vitachaguliwa kutoka taasisi za elimu ya juu, kimoja kitachaguliwa kutoka taasisi ya umma na kingine kutoka taasisi binafsi.

  Wabunge wanane watateuliwa na rais na wengine wanne watatoka kwenye shirika la kisiasa la baraza la mashauriano la taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako