• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda yazindua kampeni ya kuchangia damu kufuatia ongezeko la ugonjwa wa malaria

  (GMT+08:00) 2019-08-28 10:05:11

  Wizara ya afya ya Uganda imezindua kampeni ya miezi mitatu ya kuchangia damu kufuatia ongezeko la ukosefu wa damu lililosababishwa na ongezeko la ugonjwa wa malaria nchini humo. Akiongea katika shughuli za uzinduzi, waziri wa nchi anayeshughulika na huduma za afya Bibi Joyce Moriku Kaducu amesema kampeni hiyo inalenga kuongeza vitengo vya damu hadi elfu 50 kabla ya mwezi Novemba kutoka vitengo elfu 25 vya damu vya sasa. Pia amehamasisha wananchi kuchangia damu ili kuokoa maisha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako