• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mchumi aona kuwa hatua ya kujibu ya China ni ya lazima kutokana na kitendo cha umwamba wa kibiashara cha Marekani

  (GMT+08:00) 2019-08-28 17:49:55

  Baada ya Marekani kutangaza kuongeza ushuru kwa asilimia 10 dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 300 zinazouzwa nchini Marekani, China imelazimika kutangaza hatua ya kujibu kuanzia tarehe 23. Baada ya hapo tarehe 24 Marekani ikatangaza kuzidi kuongeza ushuru kwa bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 550, na kufanya mgogoro wa uchumi na biashara kati ya China na Marekani kuzidi kupamba moto. Mchumi maarufu wa Japan ambaye pia ni mtafiti na mkurugenzi wa Taasisi ya uwekezaji wa biashara ya kimataifa ya Japan ITI Enara Noriyoshi anaona kuwa, China inachukua hatua ya kujibu kutokana na kitendo cha umwamba wa kibiashara cha Marekani.

  Akiongea na mwandishi wa habari Bw. Noriyoshi amesema, kutokana na kuzidi kupamba moto kwa mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani, bei ya bidhaa zinazohusika nchini Marekani imepanda, na maisha ya kawaida ya wananchi wa Marekani yameathiriwa vibaya. Aidha kupungua kwa uwekezaji wa China nchini Marekani pia kumedhuru utoaji wa nafasi za ajira nchini Marekani. Anasema:

  "Mgogoro wa kiuchumi kati ya China na Marekani si kama tu umeiathiri China, bali pia imedhuru wananchi na kampuni za Marekani, wamarekani hawataweza kununua bidhaa kwa bei nafuu kama ilivyokuwa zamani wakati wa Sikukuu ya Krismasi, na shughuli za uendeshaji wa kampuni zimeathiriwa vibaya."

  Bw. Noriyoshi pia ameeleza kuwa, Marekani iliwahi kuiunga mkono China kujiunga na Shirika la Biashara Duniani WTO, na kuikaribisha China kujiunga na utaratibu wa sasa wa uchumi duniani, ili kuhimiza ukamilifu na maendeleo ya mfumo wa uchumi na biashara duniani. Lakini sasa Marekani inatoa malalmiko na kulikosoa shirika hilo, wakati huo huo inajaribu kuzishinikizia nchi zinazohusika kwa njia ya kuongeza ushuru dhidi ya bidhaa, hatua hii ya Marekani haiwezi kukubalika. Anasema:

  "Mikwaruzano ya kiuchumi na kibiashara kati ya China na Marekani inamaanisha kuwa usimamizi wa uchumi na biashara wa dunia umeingia katika kipindi cha mageuzi na mpito, na utaratibu wa aina mpya wa usimamizi wa uchumi na biashara utaanzishwa katika siku za usoni."

  Kwa maoni ya Bw. Noriyoshi, mgogoro wa biashara kati ya China na Marekani hautaweza kutatuliwa ndani ya muda mfupi. Hivi sasa dunia nzima iko katika kipindi cha mabadiliko ya uundaji mpya wa utaratibu wa usimamizi wa dunia. Ingawa China inakabiliwa na matatizo makubwa, lakini kutokana na mipango mbalimbali ya China ikiwemo Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" na Maonesho ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa ya China, katika siku za baadaye China itachangia busara na nguvu nyingi zaidi za China katika mchakato wa mageuzi na ujenzi wa utaratibu wa aina mpya wa usimamizi wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako