• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping wa China akutana na waziri mkuu wa Uzbekistan

  (GMT+08:00) 2019-08-28 20:10:23

  Rais Xi Jinping wa China amekutana na waziri mkuu wa Uzbekistan Bw. Abdulla Aripov na kusisitiza kuwa China na Uzbekistan zinapaswa kuendelea kuhimiza ujenzi wa pamoja wa hali ya juu wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa maendeleo ya kitaifa, na kupanua maeneo mapya ya ushirikiano wa utamaduni, na China inakaribisha Uzbekistan kuwa mgeni rasmi katika Maonyesho ya pili ya kimataifa ya bidhaa zinazoagizwa na China kutoka nchi za nje.

  Bw. Aripov amesema rais Shavkat Mirziyoyev ameanzisha taasisi ya kitaaluma ili kushirikiana na China kuendeleza mkakati wa maendeleo, kuhimiza ushirikiano wa "Ukanda Mmoja, Njia Moja", kupanua mawasiliano yasiyo ya kiserikali na kibinadamu, kuimarisha urafiki wa jadi, na Uzbekistan inaunga mkono China kulinda mamlaka, usalama na umoja wa taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako