• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Balozi wa China Musmbiji awataka wanafunzi kuchangia maendeleo ya nchi yao baada ya kurudi kutoka masomoni China

  (GMT+08:00) 2019-08-28 20:15:00

  Balozi wa China nchini Msumbiji Su Jian amewahimiza wanafunzi zaidi ya 90 wa Msumbiji wanaokuja kusoma nchini China kuchangia ujenzi wa Msumbiji baada ya kurudi kutoka masomoni.

  Akiongea kwenye sherehe ya kuwaaga wanafunzi wao, Balozi Su amesema anatarajia kuwa katika siku zijazo wataendeleza kazi zao kwa kuikumbuka nchi yao, na kuwataka wachangie zaidi kwenye ujenzi na maendeleo ya nchi yao.

  Wanafunzi hao wanaokuja masomoni nchini China, watasomea masomo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uhandisi wa ujenzi, mashine, uchumi, biashara, kilimo na matibabu, ambayo yote ni muhimu sana kwa maendeleo ya uchumi na kijamii nchini Msumbiji.

  Kwa sasa kuna makampuni zaidi ya 100 yaliyowekeza nchini Msumbiji, yakiwa na thamani ya dola za kimarekani bilioni 7.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako