• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa wito wa kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji ili kukabiliana na tishio la ugaidi

  (GMT+08:00) 2019-08-28 20:15:14

  Naibu balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Wu Haitao amesema nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zinapaswa kuwa macho juu ya tishio la ugaidi linaloisukumbua dunia nzima, jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuimarisha ushirikiano wa kiutendaji, ili kukabiliana na tishio la ugaidi kwa pamoja.

  Balozi Wu amesema hayo jana alipohudhuria mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu suala la ugaidi linalotishia amani na usalama wa dunia. Amesema Kundi la IS bado ni kundi la kigaidi linaloitishia dunia nzima, Umoja wa Mataifa na Baraza la Usalama zinapaswa kuimarisha kazi ya uratibu katika kupambana na ugaidi. Pia amesema Jumuiya ya Kimataifa inatakiwa kutatua masuala makuu kwa njia ya kisiasa, na kuzisaidia nchi wanachama zitimize maendeleo endelevu.

  Ameongeza kuwa China ni nchi muhimu katika mapambano dhidi ya ugaidi, na inapenda kushirikiana na nchi nyingine katika kukabiliana na tishio la ugaidi na kulinda kwa pamoja amani na utulivu wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako